Monday, September 15, 2014
KIKAO cha 53 chaanza nchini Iran
KIKAO cha 53 cha Taasisi ya Kisheria na Mashauriano ya Asia na Afrika kimeanza hapa Tehran kwa kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wageni kutoka nchi za nje.
Wawakilishi wa nchi za Asia na Afrika ambao wako hapa Tehran kwa minajili ya kushiriki kwenye kikao cha 53 cha ALCO watawasilisha mitazamo yao kuhusu mabadiliko yaliyojitokeza katika sheria za kimataifa.
Wawakilishi wa nchi 47 wanaohudhuria kikao cha 53 cha ALCO wanajadili na kubadilishana mawazo kuhusu masuala muhimu na mabadiliko mapya katika sheria za kimataifa.
Kikao maalumu cha kuchunguza misimamo ya kuchupa mipaka na ugaidi kitafanyika pia pambizoni mwa mkutano wa 53 wa ALCO hapa Tehran.
Mkutano huo utajadili na kuchunguza pia kadhia nyingine muhimu kama namna ya kuamiliana na wakimbizi, kufukuzwa Wapalestina katika nchi yao na hatua nyingine za utawala wa Kizayuni wa Israel zinazokiuka sheria za kimataifa hususan Azimio la Nne la Geneva la mwaka 1949
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment