![]() |
| Wananchi nchini Nigera wakikimbia makazi yao |
Taarifa kutoka kaskazini mashariki mwa Nigeria zinasema kuwa, maelfu ya raia katika jimbo la Adamawa wameyakimbia makazi yao hasa baada ya kuripotiwa kwamba, wanamgambo wa Boko Haram wanajipanga kufanya mashambulio katika maeneo hayo.
Taarifa hizo zinajuza kuwa wakazi wote wa maeneo hayo wamekimbilia milimani na katika mji wa Mubi baada ya jeshi kufanya operesheni kwenye mji wa Madagali lakini kushindwa kuwarejesha nyuma wanamgambo hao.
Katika wiki zilizopita kundi hilo limeteka miji na vijiji kadhaa nchini Nigeria, suala lililofanya eneo lililo chini ya udhibiti wao kuwa kubwa zaidi huko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

No comments:
Post a Comment