![]() |
| Rais wa Kenya Uhuru Kenya |
KENYA imesema kuwa itatoa msaada wa shilingi milioni
87 kwa Sierra Leone, Guinea na Liberia ili kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa
wa ebola.
Hayo yalisemwa
jana na Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta. Rais wa Kenya amesema kuwa nchi yake
imetoa mchango huo katika fremu ya sera za nje za Kenya za kushirikiana na nchi
nyingine za Kiafrika.
Rais Uhuru Kenyatta pia amewahakikishia
Wakenya kuwa uchunguzi wa mipakani utaendelea ili kuhakikisha kuwa raia wa nchi
hiyo wanalindwa na maambukizi ya ebola. Rais Kenyatta aliwahi kusema kuwa Kenya
haitazitelekeza nchi za magharibi mwa Afrika zilizoathiriwa na homa hatari ya
ebola.

No comments:
Post a Comment