Thursday, September 4, 2014

MISRI yazuia kuoneshwa kwa kipindi cha densi ya jadi


Wachezaji wa ngoma ya jadi nchini Misri
BODI ya kidini ya misri, imetoa fatwa kukataza uonyeshaji wa kipindi kilichoanzishwa kwenye televesheni nchini humo kuonyesha densi ya jadi ya wanawake wa misri ya kunengua viuno almaarufu 'belly dance'.

Ngoma hiyo inayofanana na chakacha ya waswahili imechezwa tangu zama za kale na imenakiliwa hata katika enzi za ma-pharoah katika nchi hiyo ya Misri.
Ni densi ambayo isingekosekana kwenye sherehe muhimu. Harusi au burudani nyenginezo.
Maelfu ya watalii wanaoitembelea Misri hupenda kwenda kuona inavyochezwa lakini mnamo siku za hivi karibuni wasichana kutoka sehemu nyingi duniani hasa ulaya na hata uchina wameripotiwa kwenda Misri kujifundisha jinsi ya kucheza densi hiyo.
Ni ajabu kuwa sasa imekuwa maarufu katika mataifa ya kigeni kuliko Misri kwenyewe ambako haichezwi ovyo ovyo hadharani.


No comments:

Post a Comment