Saturday, September 13, 2014

MOHAMUD asema yuko fiti kugombea uraisi 2016


Hassan Sheikh Mohamud waSomalia
.

RAIS Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia amesema kuwa, atagombea uchaguzi mkuu wa  rais wa mwaka 2016.

 Rais Mohamud ameyasema hayo huko Mogadishu, mji mkuu wa nchi hiyo kwenye hafla ya kujadili mafanikio na changamoto katika miaka yake miwili ya kwanza ya uongozi wake, ambapo pamoja na mambo mengine amewataka Wasomalia kushiriki katika uchaguzi huo.
 Amesema na hapa ninamnukuu: "Mwaka 2016 kutakuwa na uchaguzi wa rais ambapo kila raia wa Somalia atakuwa na haki ya kushiriki uchaguzi huo kwa ajili ya kuwania nafasi ya urais. Nikiwa kama raia wa Somalia, nami nina haki ya kugombea nafasi hiyo." Mwisho wa kunukuu. Hata hivyo bado haijafahamika uchaguzi huo utakuwa na muundo gani hasa kwa kutilia maanani matatizo ya kifedha yanayoikabili serikali kuu na kadhalika ukosefu wa usalama katika maeneo mengi ya nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

No comments:

Post a Comment