Monday, September 15, 2014

SERIKALI KUU yakwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo


Meja wa manispaa ya Morogoro Amir Nondo

HALMASHAURI ya wilaya ya Morogoro imebainisha kuwa
 kutotekelezeka kwa miradi ya maendeleo ya jamii kwenye
 halmashauri hiyo kunatokana na serikali kuu kubadilisha
 vipaumbele na bajeti zake.


 Hayo yalisemwa na Afisa mipango wa halmashauri hiyo Heri
 Kuria kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wakati akijibu baadhi
 ya changamoto zilizoibuliwa na Mtandao wa jinsia nchini TGNP
 kwenye majumuisho ya uchambuzi wa bajeti na utekelezwaji wa
 sera katika Halmashauri.


 Awali mwakilishi wa TGNP Rebeka Mjema alitaja baadhi ya
 changamoto zilizobainika katika ufuatiliaji huo ukiwemo
 mradi wa kilimo cha umwagiliaji Kiroka uliokwamia katikati
 na kuamsha chuki baina ya wanachinchi.

 Alisema sambamba na mradi huo kunamiradi mingine
 imeutekelezwa njiani na haitolewi taarifa kwa wanachi hivyo
 kuanza kuharibika jambo ambalo ni hasara kwa wananchi na
 Taifa kutokana na fedha zao kupotea bila tija.


No comments:

Post a Comment