Monday, September 15, 2014

POLISI Uganda wakwamisha jaribio la Al-shabab


Askari polisi nchini Ugandawakiwa katika doria

 POLISI nchini Uganda wanasema kuwa wamekamata kiasi kikubwa cha vilipuzi walipokuwa wakifanya operesheni ya kutibua jaribio la shambulizi la kigaidi la wanamgambo wa al-Shabab.

Hadi sasa, watu kumi na tisa wamekamatwa na polisi na wanahojiwa kuhusiana na nia yao kutekeleza vitendo vya kigaidi, kulingana na msemaji wa polisi.
Wiki iliyopita, ubalozi ya Marekani mjini kampala ulionya kuwa kulikuwa na uwezekano wa shambulizi la kulipiza kisasi mauaji wa kiongozi wa kundi hilo la Alshabab.
Uganda inalaumiwa kwa kutoa majeshi yake kupigana chini ya nembio ya Umoja wa Afrika Amisom.

No comments:

Post a Comment