![]() |
| Steven Sotlof |
WAPIGANAJI wa
dola ya Kiislam IS wamesambaza picha za video katika mitandao kwa lengo la
kuonyesha kuchinjwa kwa mwandishi wa habari raia Marekani Steven Sotloff ambaye
ni mmoja wa mateka wanaoshikiliwa na wapiganaji hao.
Mwandishi huyo Sotloff, mwenye umri
wa miaka 31 ambaye alitekwa na wapiganaji hao mwezi August mwakajana.
Mwezi uliopita Sotloff alionekana mwishoni
katika picha za video zilizoonyeshwa kuhusiana na kuchinjwa kwa mwandishi
mwingine wa Marekani James Foley.
Wapiganaji hao wa katika picha hizo
pia wameonekana wakimtishia kumuua mateka mwingine anayedhaniwa kuwa ni raia wa
Uingereza.
Baada ya mauaji ya mwandishi wa
awali Foley, mama mzazi wa mwandiashi wa Sotloff alitoa ombi maalumu kwa
kiongozi wa wanajeshi hao Abu Bakr al-Baghdadi kutoa muua mtoto wake.
Msemaji wa Ikulu ya White House Josh
Earnest amesema kuwa maofisa wa Marekani wanaendelea na uchunguzi wa ripoti
hiyo.
Marekani hivi karibuni ilifanya
mashambulizi ya anga dhidi ya IS nchini Iraq.

No comments:
Post a Comment