![]() |
| Chinedu Obasi |
SHIRIKISHO la soka Nigeria limesesema litaishitaki klabu ya
Schalke ya Ujerumani kwa Fifa baada ya klabu hiyo kukataa kumruhusu mshambulizi
Chinedu Obasi kushirki michuano ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika mwaka
2015.
Hata hivyo klabu ya Schalke imesema
kuwa sababu ya kukosa kumruhusu mchezaji huyo kuondoka ni kwamba pasi yake ya
usafiri iko katika ubalozi huku viza yake ikitayarishwa kabla ya kuanza kwa
michunao ya klabu bingwa Ulaya.
Nigeria ambao ni mabingwa wa Afrika,
watamenyana na Congo mnamo tarehe sita Septemba.
Siku nne baadaye watatoana kijasho na Afrika
Kusini. Nigeria imekasirishwa naSchalke kuhusu mchezaji wake Obasi.

No comments:
Post a Comment