Wednesday, September 17, 2014

RAIS Obama atuma wanajeshi 3,000 Afrika Magharibi kusaidia Ebola



Rais Barack Obama

 RAIS wa Marekani Barrack Obama ametangaza mpango wake wa kuwatuma wanajeshi  3,000 Afrika Magharibi kama njia mojawap ya kusaidia katika vita dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola.

Rais Obama ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za dharura kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Ebola Magharibi mwa Afrika ambao unaenea kwa kasi sana.
Bwana Obama amesema kuwa iwapo mlipuko wa maradhi hayo haukomeshwi kwa sasa, mamia ya maelfu ya watu wataambukizwa na yatakuwa tishio kwa usalama wa dunia.

No comments:

Post a Comment