Saturday, September 13, 2014

SERIKALI ya China yaahidi mabilioni miradi ya maendeleo




Balozi wa China nchini Tanzania kulia
SERIKALI YA CHINA imeahidi kushirikiana na Serikali ya
 Tanzania katika miradi ya maendeleo ikiwemo kutoa
 fursa  za nafasi za masomo na ajira kwa wanafunzi
 wanaohitimu  elimu ya juu katika vyuo vikuu vya
 Tanzania  .



 Hayo yameelezwa na  meneja wa kampuni ya Linghang
 group  ya  nchini China  profesa Daniel
 Chieh  wakati  akizungumza  na wanafunzi wa
 chuo kikuu cha Mzumbe katika semina maalumu ya mahusiano
 baina ya china na chuo hicho.
 Katika semina hiyo Profesa Chieh alisema China ipo tayari
 kutoa fursa kwa vijana wapendao kushiriki na kusoma fan
 mbalimbali nchini mwao ikiwa ni hatua mojawapo ya kuwajengea
 uwezo masuala ya elimu na ajira.

 Makamu mkuu wa chuo cha mzumbe Prof Joseph Kuzilwa alisema
 ushirikiano huo utaanzisha mfuko maalumu wa kuwajengea uwezo
 wanafunzi nchini  katika sekta mbalimbali zikiwemo za
 ujasiliamali sekata ambayo ni nguzo ya maendeleo China.

 Aidha aliwataka wanafunzi kutobweteka na msongamano wav yeti
 kwenye makabati badala yake watumie muda mwingi kutafsiri
 elimu wanazopata vyuoni katika maisha yao ya kilasiku kama
 ilivyo tokea kwa wasomi nchini China.


No comments:

Post a Comment