![]() |
| Nyumba iliyoathiriwa na mabomu ya Mbagala |
MKUTANO kati ya waandishi habari na Waathirika wa Mabomu
Mbagala, ambao umefanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mbagala Kuu
,jijini Dar-Es-Salaam mapema leo .
Waathirika hao wapatao 1,361 kati yao 25 wameishapoteza maisha kutokana na athari za mabomu hayo.
Mlipuko huo wa mabomu ni tukio lililotokea tarehe 29 April mwaka 2009,majira ya saa sita kasa robo katika eneo la mbagala kuu,hii ni baada ya mabomu hayo kulipuka katika ghala la silaha ya kambi ya ulinzi ya jeshi ya jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania(JWTZ) namba 671 kj.
Mabomu hayo yaliyokua yanalipuka kwa mfululizo yalisababisha vifo,kujeruhi,kuharibu makaazi na mali za watu kuharibiwa vibaya na kwa upande wa afya athari zilizojitokeza ni maradhi ya TB ama kifua kikuu,upofu wa macho,saratani,tezi yamkojo na kadhalika.

No comments:
Post a Comment