Saturday, September 13, 2014

CHADEMA Kilosa wakamata makada wa CCM



UONGOZI mpya wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA jimbo la Kilosa kati mkoani Morogoro umeanza umeanza kazi kwa kukinasa makada wanne wa chama cha Mapinduzi CCM kata ya Magomeni wilayani humo wakiwa na nyaraka za serikali kinyume cha sheria wakiandikisha majina ya watu.


Wakizungumza na waandishi wa habari,mwenyekiti wa Chadema wilayani Kilosa Seleman Simba na Katibu wa jimbo la Kilosa kati Chadema Mussa Ngongi kwa nyakati tofauti walisema makada hao wa ccm waliwanasa Septemba 7 mchana wakiendelea na zoezi hilo la uandikiashaji

kisheria zoezi lilipaswa kufanywa na maafisa watendaji wakishirikiana na wenyeviti wa vitongoji,tofauti na hivyo uongozi wa halmashauri kwa makusudi umegawa kwa makada wa ccm vitabu vya kuandikisha majina ya wakazi vitongojin…kwa mtazamo wetu hii inafanyika makusudi kuiandalia ccm ushindi katika chaguzi zijazo”Alifafanua Ngongi.

Viongozi hao walisema mbali na zoezi hilo kushitukiwa kwa kupewa makada wa ccm kuliendesha badala ya watumishi wa serikali,pia zoezi hilo walilishitukia kutokana na lilivyokuwa likiendeshwa kwa ubaguzi likiwatenga wenye itikadi tofauti na ccm na wenye misimamo tofauti.

Walisema kilicho washangaza zaidi ni hata baada ya suala hilo kufikishwa kituo kikubwa cha polisi wilayani humo,Polisi akiwemo mkuu wa kituo hicho walilazimisha suala hilo kumalizwa kwa mazungumzo badala ya sheria kufuta mkondo wake.

Katika ufafanuzi wa zoezi hilo,mkurugenzi wa halamashuri hiyo Idd Mshili mbali na kukiri kuwepo kwa zoezi la utambuzi wa wakazi unaofanyika kila baada ya miezi mitatu,alikana halmashuri hiyo kutoa kazi hiyo kwa makada wa ccm zaidi ya maafisa watendaji anaowatambua kisheria.

Mkurugenzi Mshili alisema kama kunawatu nje ya maafisa watendaji wanaandikisha watu ni kinyume na kosa kisheria kufanyika hivyo.


No comments:

Post a Comment