![]() |
| Waziri wa mambo ya nje wa Iran (katikati)akiwasili Newyork Marekani |
MUHAMMAD JAVAD ZARIFU, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amewasili mjini New York kwa minajili
ya kushiriki kwenye mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na katika
duru mpya ya mazungumzo kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kundi la 5+1.
Katika safari yake
hiyo huko New York, Muhammad Javad Zarif ameongozana na Abbas Araqchi Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje anayehusika na masuala ya kimataifa, Majid Takhte
Ravanchi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayehusika na masuala ya Ulaya na
Marekani, Hamid Baid Nejad, Mkurugenzi wa masuala ya kisiasa na kimataifa na
maafisa wengine wa kisiasa, kisheria na vyombo vya habari wa Wizara ya Mambo ya
Nje ya Iran.
Duru ya saba ya
mazungumzo kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi wanachama wa kundi la
5+1 itafanyika kesho Alhamisi katika ngazi ya Manaibu Mawaziri wa Mambo ya Nje.
Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na bi Catherine Ashton Mkuu
wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya pia watashiriki kwenye mazungumzo hayo ya New
York.

No comments:
Post a Comment