RAIS Robert
Mugabe wa Zimbabwe amekosoa vikwazo ilivyowekewa Russia na Magharibi kuhusiana
na mgogoro wa Ukraine na kusema kuwa ni kinyume cha sheria.
Mugabe amesema vikwazo
vinapasa kuidhinishwa kwanza na Umoja wa Mataifa na kwamba vile ilivyowekewa
Russia na nchi za Magharibi havijapasishwa na umoja huo.
Rais Mugabe na Sergei
Lavrov Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia aliyeko ziarani nchini Zimbabwe jana
walisaini makubaliano ya uwekezaji ya dola bilioni tatu, ambapo Russia
itachimba madini ya platinamu huko Zimbabwe.
Rais Mugabe amelaumu pia vikwazo vipya vya
Magharibi dhidi ya Russia ambavyo vimelenga katika sekta za benki, nishati na
ulinzi.
Kwa upande wake Waziri wa
Mambo ya Nje wa Russia amesifu nafasi ya Afrika katika nidhamu mpya ya
ulimwengu sambamba na jitihada za Moscow za kuimarisha uhusiano na waitifaki
wake wa Afrika.
Amesema kuwa Afrika ni
moja ya nguzo za ukuaji wa mfumo wa ulimwengu. Mgogoro wa Ukraine umesababisha
kuvurugika uhusiano kati ya Russia na nchi za Magharibi. Marekani na
Umoja wa Ulaya zinaituhumu Russia kuwa na ina mkono katika mgogoro huko
mashariki mwa Ukraine,tuhuma ambazo zimekanushwa na Moscow.

No comments:
Post a Comment