MASHINDANO ya
kutafuta klabu bingwa ya bara la ulaya
katika mchezo wa soka ilianza jana huku timu kadhaa zikishuka katika viwanja
mbalimbali ili kuanza kuzitafuta point tatu muhimu.
Mabingwa watetezi Real Madrid iliialika FC Basel katika uwanja wa Benabeu na kuanza vyema mbio za kutetea taji hilo kwa kuwafunga wapinzani wao kwa jumla ya mabao 5-1 huku washambuliaji wake wote wakiweza kuzifumania nyavu za wapinzani wao.
Katika viwanja vingine Liverpool imeutumia vyema uwanja wake wa nyumbani na kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Ludogorets Razgrad na kushuhudia mwanzo mzuri wa mshambuliaji Baloteli aliyefunga moja ya mabao hayo mawili.

No comments:
Post a Comment