Friday, September 19, 2014

RUSHWA kwa viongozi wa kata ndio chanzo cha migogoro ya ardhi



Mkurugenzi mkuu wa Takukuru Dk Edward Hosea
VIONGOZI wa serikali  ngazi ya vijiji na kata  Tarafa ya Magole Wilayani Kilosa wametajwa kuwa na 'Kansa' ya rushwa katika utumishi wao ambayo ni chanzo kikuu cha migogoro ya ardhi kwa ulafi wa kujipatia utajiri kwa njia ya mkato.


Akifungua mdahalo ulioandaliwa na asasi ya DIRA kwa ushirikiano na Foundation For civil society FCS Afisa tarafa ya Magole Moses Nchimbi alisema udhaifu huo kwa viongozi hao umekuwa chanzo cha umasikini kwa jamii na serikali kwa jumla.

Nchimbi alisema wapo baadhi wa wenyeviti walitoa ufumbuzi juu ya swala la migogoro ya ardhi kwa kufuata sheria za ardhi lakini ipo haja kuziongezea nguvu kwa kupunguza baadhi ya watendaji wazimbe na changamoto za mara kwa mara zinazotokana na migogoro ya ardhi.

Hata hivyo mwezeshaji na mshauri wa masula ya ardhi Rajabu Husen na diwani wa maguha,Dicksoni Magoma walikili sera na sheria zikiwemo za ardhi kutotekelezwa kawa makudi ya kujiingizia kipato kutoka kwa jamii.


Mbali na hayo pia alisema hakuna ushirikiano wa dhati kati wananchi na  viongozi wao ambapo tayari baadhi ya asasi za kiraia ikiwemo Dira zimejitoa muhanga kupambana na hali hiyo.








No comments:

Post a Comment