Friday, September 19, 2014

UDHAIFU wa serikali chanzo cha umaskini



ONGEZEKO la umasikini nchini linatokana na udhaifu wa serikali iliyopo madarakani katika kutekeleza viashiria vya utawala bora kikiwemo cha utawala wa sheria,uwazi na ukweli,ushirikishaji,uwajibikaji,usawa na uadilifu kwa jamii.


Hayo wamebainishwa kwenye mafunzo ya Utawala bora,Bajeti na ufuatiliaji wa rasilimali za umma kwa waraghibishi ngazi ya jamii na mafunzo hayo kwa Madiwani,viongozi kutoka halmashauri maafisa watenjaji vijiji na kata mjini hapa TGNP.

Katika mafunzo ya walaghbiishi Thelesia Berege na Hawa Saleh kwa nyakati tofauti walisema viongozi vijijini wamegeuka miungu watu wasiotaka kuhojiwa jambo lolote licha ya kukiuka sheria,taratibu na kanuni za utawala.

Walisema kutokana na vitisho hivyo wanachi wamekuwa waoga kuhoji mamsuala muhimu kwa maendeleo yao huku fedha za umma kwa ajili ya shuguli za maendeleo zikiwa hazijulikani.

Mwezeshaji katika mafunzo hayo mtafiti na mshauri wa mambo ya kisiasa na utawala bora kutoka taasisi ya ‘Diligent international colsult Ltd’(DICL), Godlisten Moshi alisema ni haki kisheria kwa  mwanchi kudai taarifa serikalini na kuzifanyia kazi.


Alisema wananchi wanapaswa kuamka na kudai taarifa hizo badala ya kuogopa kuzidai kwani inaongeza mwanya kwa viongozi kuendelea kuhujumu mali za umma kwa urahisi na kukwamisha maendeleo yao katika jamii.











No comments:

Post a Comment