Friday, July 31, 2015
UHAMIAJI nchini Tanzania yatoa onyo kwa raia wa kigeni
IDARA ya Uhamiaji nchini Tanzania imetoa onyo kwa raia wa kigeni watakaobainika kuwa na vitambulisho vya kupigia kura baada ya kuwagundua raia zaidi ya 2,000 wa kigeni wenye vitambulisho hivyo katika msako unaofanywa na maofisa wao kwenye miji iliyo mipakani.
Idara hiyo imesema tayari imeshaanza kuwachukulia hatua za kisheria raia hao ikiwa ni pamoja na kuwanyang’anya vitambulisho hivyo, kuwaondoa nchini baadhi na wengine kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Wakati huo huo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC) imeongeza siku nne zaidi kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Mfumo wa Kielektroniki (BVR).
Kwa ratiba iliyotolewa awali na NEC, leo ndio ilikuwa siku ya mwisho kwa wakazi wa jiji hilo kujiandikisha kwenye daftari hilo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema wameongeza siku hizo kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi ulioonekana katika vituo mbalimbali vya kujiandikisha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment