![]() |
Watumishi wa Halmashauri ya Kilombero |
HALMASHAURI ya wilaya ya Kilombero imeanza maandalizi ya ujenzi wa
makao makuu ya Mkoa mpya wa Ulanga kwa kutenga eneo ekari 100
.
Maandalizi hayo yamefahamika katika
kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya(DCC)mjini Ifakara wakati mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero Azimina Mbilinyi akiwasilisha
hoja ya ya kuugawa mkoa wa Morogoro zilimo wilaya ya Ulanga na Kilombero ili
kusogeza huduma za kijamii na maendeleo karibu na wananchi.
Mbele ya mwenyekiti na kaimu mkuu wa
wilaya ya Kilombero ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Ulanga Christina Mdeme,
Mkurugenzi Azimina alisema uamuzi huo ulijumuisha eneo linalopakana na kijiji
cha Kapolo,Kikwawila,Lungongole na Katindiuka unakuaja baada ya kuamuliwa makao
makuu ya mkoa huo mpya kuwa wilayani Kilombero.
"Eneo hili litahusisha ujenzi
wa Ikulu ndogo na usalama wa Taifa ekari 50 kati,ekari 30 ujenzi wa ofisi za
uhamiaji,takukuru,mahakama na polisi na ekari 20 zitakuwa akiba kwa ajili ya
ujenzi wa taasisi nyingine za serikali kwa kadri
itakavyohitajika"Alifafanua Azimina.
Alisema alisema ombi la moka wa
morogoro kugawanywa lilitokana na mkoa huo kuwa mkubwa, changamoto ya jiografia
yake, changamoto ya upatikanaji huduma za maendeleo na ufanisi wake katika
utawala na usimamizi wa shughuli za maendeleo.
"amkoa huu utakaokuwa na
ukubwa wa Kilomita za eneo 39.4 utakuwa na watu 673,080 ukigawanyika katika
wilaya tatu ikiwemo ya Ulanga,Kilombero na Malinyi halmashauri nne ikiwemo ya
Ulanga,Malinyi,Kilombero na halmashauri ya mji wa Ifakara na majimbo
manne"alisema Mkurugenzi huyo.
kwa mujibu wa mkurugenzi huyo fursa
za wilaya hizo na mkoa zitakuwa ni ardhi,jiografia,miundombinu,uchumi na huduma
za kijamii akifafanua kuwa wilaya ina kilomita za mraba 14,918 na watu 407,880
wenye kaya 94,604.
Akipongeza mpango mkakati huo kaimu
mkuu wa wilaya hiyo Christina,aliwapongeza wajumbe kwa kupitisha kwa
kauli moja ya kufanya Ifakara kuwa makao makuu ya mkoa mpya na kusema mkoa mpya
umekidhi vigezo vyote vya kutakiwa kuwa mkoa isipokuwa kigezo kimoja cha kuwa
na tarafa chache.
Christina alisema mkoa utakuwa
na kata 66,vijijiji 202,kilomita za mraba 39,483 na watu 673,080 na tarafa 12
na kusema lengo la kugawa mkoa ni kusogeza huduma kwa wananchi na kuwaletea
karibu maendeleo yao.
Ifakara kuwa makao makuu ya mkoa
mpya na kusema mkoa mpya umekidhi vigezo vyote vya kutakiwa kuwa mkoa isipokuwa
kigezo kimoja cha kuwa na tarafa chache.
No comments:
Post a Comment