![]() |
Mwenyekti wa H/w Kilosa aliyesimama kati akiwa na wanafunzi |
WAKATI zoezi la uchuakuaji fomu za kuwania ubunge kutoka Tume ya Taifa
zikianza kutolewa nchi nzima,jana juzi mitaa ya kilosa kati ilifungwa kwa muda
wakati mgombea ubunge Abeid Malapakolo kupitia Ukawa akiwakilisha chama cha
wanachi CUF alipokwenda kuchukua fomu katika ofisi za Halmashauri hiyo.
Mkoa wa Morogoro una jumla ya
majimbo 11 kati ya hayo majimbo tisa wagombea wake watakuwa ni wa chama
Demokrasia na Maendeleo Chadema kupitia Ukawa na majimbo mawili likiwemo la
Kilosa na Morogoro kusini watawakilishwa na wagombea kutoka Cuf.
Mara baada ya kuchukuwa fomu
Mlapakolo alisema umati huo unatokana na watanzania kukubali mabadiliko chini ya
mwamvuli wa ukawa nakuwa lengo lao si polojo bali maendeleo ya kweli dhiidi ya
umasikini unaowakabili sasa.
“Mwalimu Nyerere alisema watanzania
wanahitaji mabadiliko wasipoyapata ndani ya CCM watayapata nje ya CCM sasa
umefika muda wa watanazina kuhitaji mabadiliko ambayo bila shaka yoyote
yatatimia mwaka huu”alisema Mlapakolo.
Alisema kuwa kama atafanikiwa kuwa
mbunge wa jimbo la Kilosa atahakikisa kuwa migogoro ya ardhi dhidi ya wakulima
na wafugaji iliyodumu kwa muda mrefu atahakikisha inapatiwa ufumbuzi wa
kudumu.
Wilaya ya Kilosa ina majimbo mawili
ya Mikumi na Kilosa kati ambapo jimbo la mikumi litawakishwa na Joseph
Haule(Profesa Jey)Chadema na Kilosa Abed Mlapakolo wote wanatokana na umoja wa
vyama vilivyoungana vya Ukawa.
Mlapakolo atachuana vikali na
wenzeke kaadhaa katika kinyang’anyilo hicho kama vile Hemed Limano wa
Democratic Party na Mbaraka Bawaziri wa CCM ambapo alisema wananchi wanakila
sababu ya kumchagua yeye kwa maendeleo zaidi kwa wana kilosa.
Idd Abdurrahman ni msimamizi wa
uchaguzi katika wilaya ya Kilosa amewataka wagombea wate kuwapa elimu wapenzi
na wanachama wao kutofanya fujo wakati wa kampeni na hata siku ya kupiga kura
kwani uchaguzi utakuwa wa uhuru na haki.
No comments:
Post a Comment