Vyombo vya habari nchini vimetakiwa
kuwa makini na kuripoti habari za uchaguzi mkuu wa mwaka huu kufuata maadili na
weledi wa taaluma hiyo ili kufanikisha uchaguzi huo kwa amani
Hayo yamesemwa leo jijini Mbeya na
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA wakati wakiwapa semina mameneja na
wamiliki wa vyombo vya habari vilivyopo kanda ya nyanda za juu kusini semina
iliyofanyika jijini Mbeya
Akizungumza katika semina hiyo wakati
wa hotuba ya kufungua semina hiyo Naibu Mkurugenzi idara ya utangazaji TCRA
makao makuu Bw. Fredrick Ntobi amewasisitiza waandishi wa habari kote nchini
kuhakikisha wanafuata maadili ya kazi zao ili kuepuka madhara yatakayoweza
kujitokeza pindi watakapotoa taarifa potofu kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu
na chaguzi nyingine zitakazofuata baada ya uchaguzi huo
"Naomba muwe makini na uandishi
wenu wa habari maana ninyi ninyi ndio mtakaofikishwa mahakamani, ninyi ndio
mtakaofikishwa The Heag, ajirini watu wenye professional (taaluma) ya habari,
hii itasaidia kuepuka kauli za uchochezi, zitawamaliza na niwahakikishie sisi
kama mamlaka tupo makini na tutafuatilia vyombo vyote vya habari" amesema
Ntobi
Kwa upande wake Mhandisi mkuu idara ya
Utangazaji TCRA makao makuu Mhandisi Andrew Kisaka amewataka washiriki
kuhakikisha wanazingatia usawa katika kutoa taarifa za uchaguzi na kuepuka
upendeleo wa baadhi ya vyama
"Unakuta CHADEMA mnawapa dakia
mbili kujieleza halafu CUF mnawapa dakika 20 hili sio sawa, hakikisha mnatoa
kipindi kilichowapa fursa sawa wagombea wote bila upendeleo
Aidha Kisaka amewaonya waandishi wa
habari kuacha kujiingiza kwenye siasa kwa kushabikia wagombea fulani na
kuingiza itikadi zao katika kuripoti habari za uchaguzi kwa kuwa itasababisha
kuwagawa wananchi na kuona kituo chako kina upendeleo jambo ambalo halitakiwi
Katika semina hiyo washiriki wamepewa
nafasi ya kuuliza ma swali na kutoa ushauri wa masuala mbalimbali
yaliyowasilishwa kwa lengo la kurahisisha utekelezaji wa mambo hayo katika
vyombo vyao vya habari wanavyofanyia kaz
No comments:
Post a Comment