Thursday, August 6, 2015

WAUMINI KKKT kumburuza mahakamani Askofu



WAUMINI wa kanisa la kiinjili la Kilutheli Tanzania KKKT dayosisi ya Morogoro wanakusudia kuiburuza mahakamani Halmashauri kuu ya Dayosisi hiyo na Asikofu wake kwa kukiuka katiba ya dayosisi hiyo na kumpitisha kwa nguvu asikofu Jacob Ole Mameo kukuendelea kuwaongoza.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti na kutoa barua ya tarehe 11/Julai kumbu namba KAM/2015/01 tunayo kwenda kwa mkuu wa KKKTnchini Asikofu Dr.Alex Malasusa na nukuu ya katiba inayoliongoza kanisa hilo Dayosisi ya Morogoro katika chaguzi,baadhi yao Gabriel Nzalayaimisi, Robert Mwanga na Maiko Loweza walisema kilichofanyika katika kura ile ni 'magumasdhi' ya kulindana.

" katika ufafanuzi wake msharika huyo alisema waliamua kumwandikia barua asikofu mkuu Dk. Malasusa kuomba ufafanuzi juu ya yaliyotokea lakini amewapuuza na sasa wanasubiri hadi Agosti 9 kwa mujibu wa siku 28 waliotoa kwa kiongozi huyo na halmashauri kuu hiyo ya dayosisi nakuwa kama hakutakuwa na la ziada watakwenda mahakamani.

katika ufafanuzi wao washarika hao walisema kura zilipopigwa kwa mara ya kwanza mbele ya asikofu mkuuDk. Malasusa, Asikofu anayelalamikiwwa Jacob Mameo alipata kura 98 hapana 68 kati ya kura zaidi ya 113 alizopaswa kupata.

walisema kura hizo zilipopigwa kwa mara ya pili na hata kwa mara ya tatu asikofu Mameo alipata kura 97 huku 71 zikimkataa jambo ambalo kwa mujibu wa katiba ya Dayosisi hiyo 2011 kufungu(vi)C kuchagua viongozi kipengele (2) hapaswi kuendelea na nafasi hiyo.

Alipotafutwa katibu wa dayosisi hiyo Mchungaji Mathias Mduma kutoa ufafanuzi wa kikatiba baada ya kukosekana ofisini,alikili kulitambua suala hilo ingawa hakuwa tayari kulitolea maelezo kutokana na siku nzima jana kuhitajika mahakamani.

hata hivyo asikofu Jacob Mameo hakutaka kuzungumzia suala hilo kutokana na suala kuwa kikatiba zaidi huku akimshauri mwandishi kuwasiliana na kati wake kwakua ndie anayeelewa na anaweza kutoa tafsiri njema.





No comments:

Post a Comment