![]() |
Prof Amina mama |
LICHA
ya dunia kukabiliwa na majanga
mbalimbali likiwemo la njaa, takwimu zinaonyesha ifikapo mwaka 2016 asilimia 50
ya wanawake duniani watakuwa wanamiliki utajiri uliopo katika jamii.
Hayo yalisemwa jijini
Dar es Salaam jana na mwanaharakati wa haki za wanawake
kutoka nchini Nigeria Profesa Amina Mama wakati wa
tamasha la Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).
Profesa Mama alisema uchambuzi
wa Kifeministi unaonyesha hakuna uhuru wowote katika sera za soko huria
zilizoletwa na taasisi za kifedha hali iliyosababisha matabaka na pengo la
walionacho na wasionacho hususani wanawake.
"Tunatambua kuwa wanawake
wamekuwa wakifanya kazi nyingi kwa muda mrefu katika mazingira magumu na
kuwasababishia msongo wa mawazo ili tu kukidhi mahitaji yao...inachochea pia
umasikini dhiidi yao lakini sasa wanaamka kwa kasi kubwa kama ilivyo nchini
Naijeria"alisema Profesa Mama.
Akiwasihi kuhakikisha
wanafanikisha mabadiliko ya kiukombozi ilikujenga usawa dhiidi wanawake lazima
wahoji na kuchambua kwa kina sera za viongozi wanaoingia madarakani
madarakani.
"mfano wa nchi katika mataifa
ya magharibi wanawake wenye kazi maofisini wanapoenda kazini huwa waacha
walezi wa watoto wao majumbani"aliongeza.
Alisema kwa sasa kuna ongezeko
kubwa la watoto ambao hawalelewi na wazazi wao, wazazi wako bize na
kutafuta pesa hivyo kuhoji nchi imepiga hatua gani tangu enzi za utumwa.
No comments:
Post a Comment