Saturday, August 22, 2015

ASIA na Afrika kuwa na idadi kubwa ya watu duniani




TAASISI ya binafsi ya ofisi ya idadi ya watu nchini Marekani imeripoti kuwa mabara ya Asia na Afrika yatakuwa na ongezeko kubwa zaidi la idadi ya watu duniani.

Taasisi hiyo imetangaza katika ripoti yake mpya kuwa hadi ifikapo mwaka 2050 mabara ya Asia na Afrika yatakuwa na asilimia 80 ya watu wote duniani.
 Ripoti hiyo imeongeza kuwa hadi ifikapo 2050 Asia itakuwa kituo kikuu cha uchumi na utamaduni katika sayari ya dunia na idadi ya watu barani Afrika itaongezeka zaidi.
Kwa mujibu wa taasisi hiyo ya Kimarekani ya idadi ya watu hadi katikati ya karne hii ya 21 nchi za Kiafrika zitakuwa miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani. Ya kwanza ni Nigeria ambayo ifikapo wakati huo itakuwa nyuma ya Marekani kwa idadi ya watu milioni moja tu.
Nchi nyengine mbili za Kiafrika ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Ethiopia. Kwa mujibu wa makisio yaliyofanywa na taasisi hiyo, ifikapo mwaka 2050 idadi ya watu wote duniani itakuwa na ongekezo la watu bilioni mbili na nusu kulinganisha na idadi ya hivi sasa. Hivi sasa China ndiyo nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani; lakini inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2050 nafasi hiyo itachukuliwa na India. Aidha Umoja wa Mataifa uliwahi kutangaza hapo kabla kuwa hadi ifikapo mwaka 2050 idadi ya watu wote duniani itapindukia bilioni 9 na milioni 700…/

No comments:

Post a Comment