![]() |
Mtambo wa Gesi Nakuru, nchini Kenya |
MRADI mkubwa wa kuzalisha nishati kwa kutumia
biogesi au gesi viumbe umeanza kufanya kazi kusini magharibi mwa Kenya, miaka
mitatu baada ya ujenzi wake kuanza.
Mradi huo wa
kwanza kabisa wa aina yake barani Afrika umejengwa mjini Nakuru na una uwezo wa
kuzalisha megawati 2.6 za umeme na utaunganishwa na gridi ya taifa na kufanya
gharama ya umeme zishuke zaidi.
Mradi huo wenye thamani ya dola za kimarekani
milioni 7.5, utapunguza gharama ya serikali inayotokana na manunuzi ya mafuta
kwa ajili ya kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme
. Gavana wa
Kaunti ya Nakuru Kinuthia Mbugua amesema mradi huo utapunguza uchafuzi wa
mazingira na kuokoa gharama za kununua lita milioni tano za diseli ambazo
hutumika kuzalisha kiwango cha umeme kama huo kila mwaka.
No comments:
Post a Comment