Friday, August 21, 2015

KASEJA asaini mkataba na Mbeya City


Juma Kaseja akionesha jezi yenye jina lake kwa wanahabari

KIPA  wa zamani wa Simba Juma Kaseja amsaini mkataba wa kujiunga na klabu ya Mbeya City Agosti 19, 2015 mbele ya meneja wake mpya Athumani Tippo na kumaliza maswali ya kuwa angecheza wapi msimu ujao.

 Taarifa hizi huenda ni pigo kwa kocha wa Mwadui FC ya Shinyanga, Jamhuri Kihwelu ambaye alikiri katika vyombo vya habari kuwa anahitaji huduma ya Kaseja kikosini mwake.
Kabla ya kusaini mkataba na Mbeya City, Juma Kaseja alikuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha zaidi ya miezi nane baada ya kuingia katika mgogoro wa kimkataba na iliyokuwa klabu yake ya Yanga na kufanya kesi hiyo kutinga mahakamani.



No comments:

Post a Comment