Thursday, November 19, 2015

BUNGE la Chad larefusha sheria ya kipindi cha hatari

Bunge la Chad
BUNGE  la Chad limerefusha kipindi cha sheria ya hali ya hatari katika eneo la Magharibi mwa nchi hiyo kutokana na mashambulizi yaliyofanywa hivi karibuni na wanachama wa kundi la kigaidi la Boko Haram ambayo yameua watu wasiopungua 12.

Wabunge 147 wa Chad wamepasisha uamuzi wa kurefusha sheria ya hali ya hatari kwa kipindi kingine cha miezi minne hadi mwezi Machi mwakani.
Jeshi la Chad limefanikiwa kuwafukuza wapiganaji wa Boko Haram katika maeneo ya magharibi mwa nchi hiyo lakini wanachama wa kundi hilo wamekuwa wakifanya mashambulizi ya kuvizia na kujilipua kwa mabomu katika maeneo ya mpaka wa nchi hiyo na Nigeria kandokando ya Ziwa Chad.
Katika safari yake ya hivi karibuni nchini Nigeria, Rais Idriss Déby wa Chad alisema kuwa kundi la Boko Haram bado halijaangamizwa kikamilifu na alitoa wito wa kuzidishwa ushirikiano wa nchi zinazopambana na kundi hilo la kigaidi huko kaskazini mwa Nigeria.

No comments:

Post a Comment