Sunday, November 22, 2015

CRIMEA giza totoro baada ya nyaya kukatika



RIPOTI kutoka Crimea zinasema kuwa jimbo hilo limebakia katika giza baada ya nyaya za umeme kutoka Ukraine kulipuliwa usiku wa kuamkia leo.

Nyaya zote nne zinazopeleka umeme katika jimbo hilo la Crimea zimekatwa sasa na kuwaacha wakaazi zaidi ya milioni mbili bila umeme.
Picha zilizosambazwa kupitia mitandao ya kijamii zinaonesha nyaya za umeme zikiwa zimetundikwa bendera ya Ukraine.
Crimea ilimegwa kutoka Ukraine na Urusi mwaka uliopita lakini utawala nchini Ukraine umekuwa ukipeleka umeme eneo hilo.
Viongozi wa jimbo hilo wanasema kuwa wamejaribu kurejesha umeme katika miji ya Simferopol, Yalta na Saky wakitumia generata lakini hautoshi.
Kwa mujibu wa naibu waziri wa Crimea, Mikhail Sheremet, hospitali na zahanati zingine za afya ndizo zilizopewa kipaombele.



No comments:

Post a Comment