MILIPUKO kadhaa imeutikisa mji mkuu wa Iraq Baghdad na
taarifa za awali zinasema kuwa, watu wasiopungua 10 wamepoteza maisha yao.
Vyombo vya usalama na duru
za hospitali zinasema kuwa, kwa uchache watu 10 wamepoteza maisha yao na makumi
ya wengine kujeruhiwa kufuatia milipuko tofauti na ufyatuaji risasi uliotokea
mjini Baghdad na katika viunga vya mji huo. Polisi ya Baghdad imetangaza kuwa,
mlipuko wa kwanza ulitokea katika soko moja mjini humo katika eneo la al-Forat.
Aidha vyombo vya usalama vya Baghdad vinasema kuwa, katika tukio jingine, watu
wasiojulikana wakiwa na silaha wameshambulia kituo kimoja cha upekuzi katika
mji wa Yusufiya uliopo umbali wa kilomita 40 kutoka katika mji mkuu huo. Wakati
huo huo jana kulitokea mlipuko wa bomu la kutegwa barabarani katika eneo la Hur
lililoko kusini mwa Baghdad na kupelekea kuuawa polisi mmoja.

No comments:
Post a Comment