![]() |
| Halmashauri ya wilaya Ulanga |
KARANTINI
iliyokuwa imewekwa na idara Afya tarafa ya Mwaya wilayani Ulanga kudhibiti
mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu uliolipuka mapema mwezi huu na kusababisha
zaidi watu 70 kukumbwa na ugonjwa huo imeondolewa baada ya ugonjwa huo
kudhibitiwa.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake,Mganga wa
kituo cha Afya Mwaya wilayani humo Dk Amos Mlai alisema ugonjwa huo uliokuwa
umelipuka mwanzoni wa mwezi huu ulisababisha karibu watu 50 kukumbwa na ugonjwa
huo na kuwa tishio katika vijiji vinavyoizunguka tarafa hiyo.
"historia ya ugonjwa huu uliletwa ma mama mmoja kutoka jijini
Dar es salaam aliyekuwa amekuja kwenye sherehe za kimila,alipofika jioni alinza
kujisikia vibaya kisha kutapika na kuharisha mfululizo...akawahi tiba hapa
kituoni lakini baada ya siku kadhaa wakaanza kuletwa watu wengine mfululizo
toka vijiji vya jirani"alisema Dk Mlai.
Dk Mlai alifafanua kuwa uchunguzi ulibaini vifaa alivyokuwa
akitumia mgonjwa wa awali vilitumika bila tahadhali na watu wengine sambamba na
nguo zake kufuliwa kwenye mto ambao maji yake hutumika kwa shughuli za kila
siku majumbani na wanachi wa vijiji vya jiarani.
"tukaamua kuviweka karantini vijiji vile na kuanza kutoa
elimu ya afya ikiwemo kuoacha kabisa kusalimiana kwa kushikana na mikono,kufunga
vyakula vinavyouzwa sambamba na pombe za kienyeji lakini pia kuzuia uingiaji na
utokaji wa mtu yeyote kijiji humo...kwa kuda wa siku tano hivi hali ile ikawa
miedhibitika"alisema dk Mlai.

No comments:
Post a Comment