![]() |
| Majaliwa K. Majaliwa |
MBUNGE wa Ruangwa Majaliwa Kassim Majaliwa
ameidhinishwa na Bunge la Tanzania kuwa waziri mkuu mpya wa Tanzania.
Bw Majaliwa amepata kura 258 kati ya 351
zilizopigwa, baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kutangazia bunge kwamba ndiye
aliyekuwa amependekezwa na Rais John Pombe Magufuli awe Waziri Mkuu.
Bw
Majaliwa, 55, amekuwa mbunge wa jimbo la Ruangwa, Jimbo la Lindi kupitia Chama
cha Mapinduzi (CCM) tangu 2010.

No comments:
Post a Comment