Sunday, November 15, 2015

WATU 127 wameuwawa nchini Ufaransa



UFARANSA imetangaza hali ya hatari na kufunga mipaka yake baada ya watu zaidi ya 127 kuuawa kwenye mashambulio kadha mjini Paris.

Watu 127 wameuawa katika ukumbi wa sanaa wa Bataclan, katikati mwa mji wa Paris.
Watu wenye silaha walishika mateka watu waliokuwa kwenye ukumbi huo kabla yao kuzidiwa nguvu na maafisa wa polisi.
Watu wengine waliuawa kwenye mlipuko uliotokea karibu na uwanja wa michezo wa taifa wa Stade de France ambako mechi ya kirafiki kati ya Ufaransa na Ujerumani ilikuwa ikiendelea.

No comments:

Post a Comment