Monday, December 28, 2015

MAGUFULI akumbushwa kuzingatia usawa wa kijinsia

MTANDAO wa mashirika yanayotetea usawa wa kijinsia na haki za binadamu(FEMACT) na wanaharakati wa demokrasia na maendeleo ngazi ya jamii (GDSS) wamemkubusha Rais Dk.John Magufuli kuzingatia usawa wa kijinsia kwa kuwakumbuka wananwake kwenye muundo wa serikali yake ya awamu ya tano.


Hayo yamo kwenye majumuisho na makubaliano ya asasi hizo yaliyotolewa kwa nyakati tofauti baada ya semina ya uboreshaji mapambano dhiidi ya unyanyasaji wa kijisinsia kupitia mikataba ya kiamatifa.

Tamko lililotolewa na viongozi mbalimbali wa asasi,mashirika na mitandao akiwemo Mwenyekiti – FemAct Abdullah Othman, Mkurugenzi mtendaji wa mtandao wa jinsia TGNP Lilian Liundi, na Mwakilishi wa mafunzo ya jinsia na Maendeleo Seleman Bishagazi walimshauri Rais kuikumbuka mikataba hiyo wakati akiunda serikali.

Kwa mujibu wa viongozio baadhi ya mikataba iliyoridhiwa ni pamoja na Tamko la Umoja wa Matifa la Haki za Binadamu(UDHR:1948), Mkataba wa Kimataifa wa Kutokomeza Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW: 1979, Articles 7: a, b na c), Mpango Kazi wa Beijing (1995), Mkataba wa Ziada wa Maputo, na Mkataba wa Nyongeza wa jinsia na Maendeleo kusini mwa Africa (SADC Gender Protocol,).

“Rais ameanza na uteuzi wa baraza la mawaziri,tulitarajia uteuzi huo kufikia 50 kwa 50 lakini katika uteuzi alioufanya tumeshuhudia wanake ni karibu asilimia 27 yaani imeshuka ikilinganishwa na seriakli iliyopita… tunaomba kunga mkono makatamko hayo katika teuzi zijazo”alifafanua Abdullah Othman na kuongeza

“tunaendelea kuhimiza usawa wa kijinsia katika teuzi zijazo kama Wabunge, Wakuu wa Mikoa na wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa na wilaya,Makatibu Wakuu na Naibu wao wizarani, Wakurugenzi,Wakuu wa taasisi na makampuni, mashirika ya umma na bodi zake bila kuusahau mhimili wa mahakama”

No comments:

Post a Comment