![]() |
| Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan |
CHAMA cha Mapinduzi kimewataka
wanachama wake visiwani Zanzibar kujiandaa kwa marudio ya uchaguzi.
Tamko hilo limetolewa
huku mazungumzo yakiendelea kutafuta suluhu ya mzozo kuhusu matokeo ya uchaguzi
wa Oktoba 25 ambayo yalifutiliwa mbali.
Wito wa wafuasi
kujiandaa kwa marudio ya uchaguzi umetolewa baada ya kikao cha kamati maalum ya
halmashauri kuu ya taifa ya CCM Zanzibar katika afisi kuu za chama Kisiwandui.
“Kikao kimewataka wana
CCM kujiimarisha, kujiweka tayari na hatimaye kujitokeza kwa wingi katika
uchaguzi wa marudio, ili kukiletea ushindi wa kishindo Chama Cha Mapinduzi
Zanzibar kuanzia Rais, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani wakati
utakapowadia,” taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo inasema.

No comments:
Post a Comment