Takwimu hizo za kipindi cha miongo miwili kutoka Idara ya Taifa
ya Takwimu zinaonyesha watoto wanaozaliwa huongezeka sana wiki 40 (miezi 9)
baada ya msimu wa sikukuu.
Hili huenda linatokana na wanandoa kutumia muda mwingi pamoja
wakisherehekea, au kulenga makusudi mwanzo wa mwaka mpya wa shule ambao huanza
mapema Septemba nchini humo.
“Ongezeko la watoto wanaozaliwa mwishoni mwa Septemba ni ishara
kwamba mimba nyingi hutungwa wiki chache kabla ya Krismasi na kuendelea hadi
siku chache baada ya Krismasi kuliko wakati mwingine wowote wa mwaka,” idara
hiyo imesema

No comments:
Post a Comment