JAPAN na Korea Kusini zimefikia makubaliano ya kihistoria kuhusu
wanawake waliolazimishwa kuhudumu katika madanguro kama watumwa wa ngono wakati
wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Mzozo
huo umeathiri uhusiano kati ya mataifa hayo mawili, Korea Kusini ikitaka
kuombwa msamaha “kwa dhati” na kutolewa kwa fidia kwa waathiriwa.
Mwafaka
wa sasa ndio wa kwanza kuhusu suala hilo tangu 1965 na umepatikana baada ya
pande zote mbili kuahidi kuharakisha mazungumzo.
Tangazo
hilo limetolewa baada ya waziri wa mashauri ya kigeni wa Japan Fumio Kishida
kuwasili Seoul kwa mashauriano na mwenzake Yun Byung-se.
Baada
ya mkutano Kishida aliambia wanahabari kwamba Waziri Mkuu Shinzo Abe ameomba
msamaha kutoka kwa “wote walioathirika”.
Wanawake
takriban 200,000 walilazimishwa kuwa watumwa wa ngono kwa wanajeshi wa Japan
wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya DUnia, wengi wao wakitoka Korea.

No comments:
Post a Comment