Monday, December 28, 2015

Azam yashinda 2-0

Azam Fc
LIGI  kuu ya Tanzania bara jana iliendelea tena kwa michezo miwili kuchezwa.
Azam Fc, wakicheza katika uwanja wao wa Azam Complex, walipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar.
Mabao ya Azam yakifungwa na Kipre Tchetche na Shomari Kapombe, huku Salum Kanoni wa Kagera akikosa mkwaju wa penati baada ya kipa wa Azam Aishi Manula kuupangua.
Na katika dimba la CCM Kirumba mjini Mwanza wenyeji Toto Afrikans walichapwa kwa bao 1-0 dhidi ya Afrikan Sport ya Tanga.

No comments:

Post a Comment