SERIKALI wilayani
Kilombero imetangaza tena kuendesha operesheni ondoa mifugo yote iliyoibuka na
kuingia kwa kasi na kutishia kuangamiza asili ya bonde la Kilombero.
Tamko hilo limetolewa
tarafani Mngeta na mkuu wa wilayaya Kilombero, mkoani Morogoro Lephy Gembe wakati akizindua nyumba ya
kulala wageni ya Sahani Lodge mali ya Sahani Masanja aliyeamua kupunguza mifugo na kujenga nyumba
ya biashara ya kulala wageni .
Dc.Gembe alisema uamuzi
huo unakuja kufuatia kuibuka ongezeko kubwa la wahamiaji katika bonde hilo ya
marufuku iliyotolewa na serilikali mwaka 2012.
"tumekaa na kamati
za ulinzi na usalama za wilaya Kilombero na Ulanga mwishoni mwa wiki na kufanya
ukaguzi kwa ndege ambapo tumejionea uharibifu mkubwa unafanyika katika bonde
hilo dhiidi ya mifugo iliyoingia kwa wingi...tumekubaliana kufanya
oparesheni"
Kwa mujibu wa Dc huyo
kwa upande wa wilaya ya Kilombero mifugo mingi imefichwa katika maeneo
yasiyofikika kwa urahisi kata ya Chisano huku upande wa wilaya mpya ya Malinyi
maeneo mengi yaliyotengwa kama ardhi oevu yamevamiwa na vigogo kwa kilimo
kikubwa.
Amewataka wafugaji
wavamizi na wakulima wanaolima katika eneo la ardhioevu kutoka haraka katika
bonde hilo kabla ya kuondolewa kwa nguvu na kutoa rai kuwa serikali
haitomwogopa mtu wakati wa zoezi hilo.
Akimzungumzia mfugaji
Sahani Masanja ambaye ameamua kupunguza mifugo yake na kuanzisha nyumba ya
kulala wageni,Gembe alisema wafugaji wengine wanatakiwa kuiga mfano wa mwenzao
kwani hivi sasa atakuwa na biashara ya kudumu hivyo kuwa na uhakika wa
kusomesha watoto wake na kufanya masuala yake ya maendeleo.

No comments:
Post a Comment