WAKULIMA wa miwa bonde la Ruhembe wilayani Kilombero,mkoa
waMorogoro wamesema wamechoshwa na wizi
unaoambatana na rushwa katika viwanda vya sukari Illovo na kuwataka wabunge wa
Chadema jimbo la Mikumi-Kilosa Joseph Haule‘Profesa Jey’,jimbo la
Ifakara-Kilombero Peter Lijualikali na Devotha Minja wa viti maalum kumwita kwa
siri Rais John Magufuli na waziri mkuu Majaliwa Kasim kuwasafisha wezi hao.
Mbele ya wabungea hao waliamua
kuunda timu ya mafanikio itakayozikabili changamoto zinazowabaili wananchi
mkoani Morogoro wakiwemo wakulima hao baadhi yao Mohamed Kapyela na Rukia
Kahuka walisema uongozi wa viwanda vya sukari ILLOVO K1 na K2 na viongozi
wa vyama vya ushirika wanashirikiana na kuwapunja malipo yao.
“kama huna kati ya 100,000 hadi
200,000 kuhonga makarai wa mizani getini lazima uibiwe kilo na kiasi cha sukari
kwenye maabara zao,ajabu ni miwa yetu pekee ambayo ni myepesi na haina sukari
lakini miwa ya kiwanda ni mizito na inasukari nyingi…jamani mwiteni Rais Dk
John Magufuli aje na huku”alsema Kahuka.
Mbele ya wabunge hao walisema mbali
na wizi huo bado hakuna ratiba inayoeleweka ya uvunaji miwa kwa wakulima
wanje,hakuna uwiano wa uingizaji miwa kindani,kuna mapunjo katika kutambua
kiasi cha sukari kwenye mua katika maabala kiwandani hapo na hata malipo
hayatoki kama inavyotarajiwa kwa kurundikiwa makato yasiyoeleweka.
Mohamed Kapyela alisema viongozi hao
wanashirikiana na uongozi wa kiwanda kupunguza kiasi cha miwa kutoka nje
kusindikwa kiwandani hapo na kusbabisha miwa mingi ya wakulima wa nje kulala
hadi zaidi ya miaka miwili bila kusindikwa na wakulima kukosa pato la kujikimu.
Aidha walisema vyama vikubwa
kikiwemo cha RCGA na KCGA amegeuka vinara kwa kukiuka katiba na
kuzibadili ili waongoze milele na wamekuwa wakitumia ukubwa wavyama hivyo
kuwakandamiza wakulima wadogo na vyama vidogo kwa kuzuia miwa isiingie
kiwandani hivyo zaidi ya tani 600 kutupwa kila mwaka bila kujali hasara.
Kutokana na vilio hivyo wabunge hao
waliazimia kupeleka hoja binafsi ya kuvilejesha serikalini viwanada
vilivyokiuka mikataba katika bunge lijalo mwezi januari Mwakani sambamba na
kumtaka waziri mkuu kufika kiwandani hapo haraka kuwashugulikia viongozi
'miungu watu' kwenye vyama kikiwemo cha Ruhembe Cane growers association-RCGA.
Mbunge Lijualikali na Devotha kwa
nyakati tofauti walipinga unyanyasaji wanaofanyiwa wakulima hao wakiahidi
kuwalinda na kuwatetea hadi hatua ya mwisho ikiwemo kurejeshewa mapunjo ambayo
wamekuwa wakifanyiwa kwa kipindi kilichopita.
“
RAIS wa Tanzania John Pombe Magufuli amewahak

No comments:
Post a Comment