Sunday, December 6, 2015

SERIKALI yabomoa nyumba 150 za wavamizi wa msitu wa serikali

SERIKALI wilayani Mvomero, mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na wakala wa huduma za misitu kanda ya mashariki  imebomoa nyumba 150 za wananchi waliovamia msitu wa kuni  wilayani humo wenye jumla hekta 12,900.

Akiongea na waandishi wa habari katika Msitu huo , Meneja wa wakala wa huduma za misitu kanda ya Mashariki Bakari Mohamed amesema kuwa wananchi walikwishatahadharishwa muda mrefu juu ya uvamizi  huo pamoja  na kuelezwa umuhimu  msitu huo kwa maisha ya binadamu na viumbe hai wengine.
Amesema msitu huo ulirasimishwa kuwa wa serikali mnamo mwaka 1953 na jitihada mbalimbali zilifanyika za utoaji wa elimu kwa umma kuhusu namana ya kutunza na kuulinda kwa maslahi ya Taifa .
 Amefafanua kuwa, baadhi ya watendaji wa idara ya misitu wilayani Mvomero wasio waaminifu wanashirikiana na wananchi kukiuka sheria , kanuni na taratuibu za uhifadhi na utunzaji wa msitu wa serikali.
Zoezi hili la kuwaondoa wavamizi hawa ni endelevu alisaema bwana Bakari Mohammed.

No comments:

Post a Comment