Sunday, December 6, 2015

Rais Putin atayarisha kituo cha kisasa cha anga

RAIS  Vladimir Putin wa Russia ametoa amri ya kutayarishwa mara moja kituo cha kisasa cha uongozi wa anga ndani ya ndege ya kistratijia iliypewa jina la Siku ya Kiyama katika kipindi cha wiki mbili zijazo.

Kituo cha habari cha Express kimeripoti kuwa, Rais Vladimir Putin wa Russia ametoa amri ya kutayarisha ndege kubwa iliyopewa jina la Siku ya Kiyama ambayo imetayarishwa kwa ajili ya vita vya silaha za nyuklia.
Mtandao wa habari wa Expresss umeongeza kuwa, wataalamu wa masuala ya kijeshi wa Russia walikuwa wamesema kuwa ndege hiyo haiwezi kuanza operesheni zake hadi mwishoni mwa mwaka huu wa 2015 lakini kufuatia mivutano iliyojitokeza baina ya Moscow na Uturuki, Rais Putin ametoa amri ya kutayarishwa ndege hiyo kwa ajili ya kuanza kutumiwa ikilazimu katika kipindi cha wiki mbili zijazo. 
Ndege hiyo inaweza kuwabeba na kuwahifadhi viongozi wa ngazi za juu wa serikali na jeshi la Russia endapo vituo vya uongozi wa masuala ya kijeshi vya nchi hiyo ardhini vitakakabiliwa na hatari. Wakati huo ddege hiyo itakuwa kituo cha uongozi wa masuala ya jeshi. Mbali na Russia ndege aina hiyo inamilikiwa na Marekani pekee duniani.








No comments:

Post a Comment