Sunday, December 6, 2015

Al-Azhar ya Misri yatahadharisha juu ya uvamizi wa msikiti wa Aqsa

Msikiti wa Aqsa uliopo Jeresalem 
TAASISI ya Al-Azhar ya Misri imetahadharisha kuhusu matokeo mabaya ya uvamizi wa mara kwa mara wa Wazayuni dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa.


Al-Azhar imetoa tahadhari hiyo   juu ya taathira za suala hilo zitakazoamsha ghadhabu na hasira ndani ya nyoyo za Waislamu wanaoishi ndani na nje ya ardhi tukufu ya Quds.
Taasisi ya Al-Azhar ya Misri imetahadharisha kuhusu matokeo mabaya ya uvamizi wa mara kwa mara wa Wazayuni dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa. Al-Azhar imetoa indhari juu ya taathira za suala hilo zitakazoamsha ghadhabu na hasira ndani ya nyoyo za Waislamu wanaoishi ndani na nje ya ardhi tukufu ya Quds.
Taarifa iliyotolewa na Al-Azhar imelaani wito uliotolewa kwa walowezi wa Kizayuni wa kuuvamia msikiti wa Al-Aqsa pamoja na mipango ya kuiyahudisha Quds tukufu na kufuta utambulisho wake wa Kiislamu.
Al-Azhar imezitaka nchi zote wapenda amani kuchukua hatua haraka iwezekanavyo ili kuzuia uchokozi na uvamizi wa kinyama wa utawala wa Kizayuni dhidi ya Quds tukufu na njama zake za mtawalia za kuliyahudisha eneo hilo. Taarifa hiyo aidha imesisitiza kwamba kadhia ya Palestina itaendelea kubaki ndani ya nyoyo na fikra za Waislamu.
Jumuiya za walowezi wa Kizayuni ziitwazo "Hekalu la Kadhai" zimetoa wito kwa magenge ya walowezi hao kuchukua hatua ya kuuvamia msikiti mtukufu wa Al-Aqsa kuanzia Jumapili ya leo. Hatua hiyo imechukuliwa sambamba na kuanza sherehe za kile kinachoitwa "Sikukuu ya Mwanga" zitakazoendelea hadi siku ya Alkhamisi










No comments:

Post a Comment