Monday, January 25, 2016

WATU 222 wafariki kwa kipindupindu nchini Tanzania

WATU 222 wamefariki kwa ugonjwa wa kipindupindu nchini Tanzania ndani ya kipindi cha miezi sita toka kuanza kwa ugonjwa huo.

Hayo yamebainishwa na shirika la  Afya la dunia, WHO,  wakati ikitokea taarifa kuhusu ugonjwa huo.
Shirika hilo limefafanua kuwa watu  14,003 wameugua kutokana na ugonjwa huo nchini Tanzania .
Hata hivyo WHO imesema kuwa Mwanzoni wa mwezi wa Januari, Tanzania ilikuwa mojawapo ya nchi 11 zilizopewa chanjo kutoka kwa WHO.
.Hata hivyo, Wizara ya Afya ya Tanzania imesema kuwa vikosi kasi vya afya vimetumwa katika sehemu vya dharura, na kuongezea kuwa kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo imeanza kupungua.


No comments:

Post a Comment