Monday, June 16, 2014

ASILIMIA 90 ya wakulima wa zao la mpunga wanatumia mbegu za kienyeji


Shamba la mpunga,Wami Lukindo, Mvomero mkoani Morogoro




ZAIDI ya asilimia 90 ya wakulima wa zao la mpunga  nchini Tanzania hutumia mbegu za kienyeji.


Hayo yamebainishwa hivi karibuni na wakala wa mbegu za kilimo nchini (ASA) katika utafiti wake  kwa kushirikiana na Kampuni ya maendeleo vijijini (  RLDC)uliokuwa na lengo la kuandaa mwongozo wa kilimo bora katika mikoa inayolima zao la mpunga kwa wingi.

Wakiongea na Mbiu ya Maendeleo jijini wataalamu toka wakala wa mbegu,wamesema kuwa,tafiti zinajuza kuwa,wakulima walio wengi wanakutana na changamoto za kukosa huduma za ugani ,kuwa na uelewa mdogo juu ya matumizi ya mbegu bora na taaluma juu ya kilimo boracha mpunga kwa ujumla.

Mbali na hayo tafitio hiyo imebaini tatizo la wakulima wengi  wanaoendesha kilimo cha umwagiliaji kukosa taaluma ya utunzaji maji shambani,matumizi yam bole ana madawa.

No comments:

Post a Comment