![]() |
Mkuu wa mkoa wa Morogoro akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro |
MKUU wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera amempa mwezi mmoja
mwenyekiti na Mkurugenzi wa Halmashuri ya Morogoro kujibu madai yote
yaliyotolewa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali za Mitaa (LAAC)dhiidi ya
halmashauri hiyo.
Agizo la Bendera kwenye baraza la
madiwani mwishoni mwa wiki linakuja baada ya ukaguzi kamati ya bunge mwaka 2013
na mkaguzi wa hesabu za serikali CAG 2012/13 kubaini mapungufu mengi katika
matumizi ya fedha za umma.
Akionyesha kupuuzwa kwa maagizi ya
CAG na LAAC, Bendera alisema mkoa hautakubaliana na dosari kama hizo za
kiutendaji katika mkoa huo.
kwa upande wake Mwenyekiti wa
halmashauri hiyo Kibena Kingu alimhakikishia mkuu huyo wa mkoa
kuwa halmashauri yake imejipanga ipasavyo kuhakikisha hoja hizo sugu
zinashughulikiwa.
Kibena alimweleza Bendera kuwa ili kutekeleza kwa vitendo changamoto hizo halamashauri imejipanga kukusanya kodi kwa zaidi ya asilimia 50 kotoka asilimia 37 mwaka 2013/2014.
Mbali na hilo pia aliongeza kuwa halmashauri imeamua kudhjibiti mianya ya uvujaji fedha za umma kwa kufuarta maelekezo ya CAG na kuhakikisha tham,ani ya fedha inakweda sambamba na kusudio katika utekelezaji.

No comments:
Post a Comment