WIZARA ya mambo ya
ndani ya nchi imesema tuhuma za rushwa zinazohambatanishwa na kazi ya usaili na
nafasi ya mkaguzi msaidizi wa uhamiaji ni hisia tu za wahusika
.
Taarifa
ya msemaji wa wizara hiyo Isaac Nantanga inasema kuwepo kwa tuhuma za
kuwepo kwa rushwa wakati wa kazi za usaili ni hisia na hazina ushahidi na kuwa
usaili ulifanywa kwa kufuata kanuni na sheria zinazosimamia ajira za utumishi
wa umma .
Nantanga
amesema waombaji zaidi walitumia haki yao ya msingi kuomba nafasi hizo na
kutokana na wingi huo wizara ilifanya mchujo wa awali na kubakiwa na maombi
10,500 ya watu wenye sifa .
Amesema
wizara ilitambua haki ya kila muombaji ya kupatiwa nafasi ya kushindaniwa
nafasi hizo ikabidi ifanyike utaratibu wa kutafuta eneo lenye nafasi kwa ajili
ya usaili huo
No comments:
Post a Comment