BEI ya vyakula katika soko la ndizi la Mabibo imeendelea
kushuka na kutoongezeka
kwa muda mrefu sasa toka kuanza kwa mwezi mtukufu wa
Ramadhani.
Wakiongea na
Mbiu ya Maendeleo mapema leo subuhi katika soko la Mabibo lililopo , Manispa ya
Kinondoni jijini Dar es salaam ,baadhi ya wanunuzi na wafanyabiashara
walimweleza mwandishi kuwa hali imetokana na uzalishaji wa mazao toka mikoa
kuongeza kwa mwaka huu.
Kwa upande
wao wananchi wanaopta huduma ya kununua vyakula mbalimbali toka sokoni hapo
wameshukuru kwani imechangia bei ya futari katika mikahawa na mamama na
babalishe katika maeneo mbalimbali ya jiji kupungua.

No comments:
Post a Comment