![]() |
| Baba akiwa na watoto wake |
MAMA mmoja amekiri kuwaua watoto wake watatu kwa sababu ya
ulemavu wao.
Tania Clarence,mwenye umri wa miaka
arobaini na miwili alikiri kosa hilo la kuwaua watoto wake watatu wakiwemo
vijana pacha wa miaka mitatu na msichana mmoja mwenye umri wa miaka minne kwa
misingi kuwa wanawe walikuwa walemavu mno.
Baba ya watoto hao alikuwa ameenda
Afrika Kusini wakati wa mauaji hayo.
Mama huyo ambaye ametoka eneo la New
Malden kusini Magharibi mwa London,alikana kufanya mauaji hayo. Watoto hao
ambao walikuwa na ugonjwa wa uti wa mgongo,walipatikana nyumbani kwao tarehe 22
Aprili mwaka huu.
Ugonjwa huo wa kimaumbile
husababisha watoto kuwa na uwezo mdogo sana wa kusongesha mwili na pia huwa
hawaishi kwa mda mrefu.

No comments:
Post a Comment