JUMUIYA ya Uchumi
na maendeleo ya maendeleo ya walemavu JUMAWATA imeziomba Taasisi mbalimbali nchini
kuwajengea msikiti na kuwachimbia kisima cha maji walemavu waishio kijiji cha
Mtamba wilayani Kisarawe , mkoa wa Pwani ili kuondokana na adha ya maji ya muda mrefu.
Akiongea na Mbiu ya Maendeleo
wilayani Kisarawe mapema leo, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mshamu Mzanda amesema,
jumawata iliamua kuomba ardhi kwajili ya shughuli za kilimo na ufugaji ili
kujikomboa kiuchumi baada ya adha ya muda mrefu ya kuishi kama ombaomba jijini
Dar es salaam toka mwaka 2004, lakini
mpaka sasa hawana uhakika wa kupata maji kwani wanatembea umbali wa kilomita
saba kufuata huduma hiyo.
Kuhusu msikiti amesema , jumuiya hiyo
ni ya watanzania wenye itikadi za ukristo na uislamu, lakini kwa upande wa
waislamu hawana sehemu ya kufanyia ibada
ilihali kwa upande wa wakristo wamepata mfadhili toka nchini Korea ambaye amewajengea kanisa na shule.
Kutokana na hali hiyo amewahimiza
wadau mbalimbali wa maendeleo kufika kijijini hapo ili waweze kuwasaidia
waislamu kupata msikiti sanjari na ujenzi wa visima vya maji.

No comments:
Post a Comment